News and Events

Kongamano La Tatu La Huduma Za Kifedha Vijijini

*****Kwa usajili wasiliana kupitia namba +255 764 668 331

Tanzania Association of Microfinance Institutions (TAMFI) ikishirikiana na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, inaandaa kongamano la Huduma za Kifedha Vijijini litakalofanyika tarehe 13 na 14 Julai, 2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya mkutano huu ni: Huduma za Kifedha Vijijini na Mageuzi ya Kilimo Tanzania. Kongamano hili linakusudia kutengeneza mazingira na kuwezesha huduma za kifedha vijijini na mageuzi ya kilimo Tanzania. Wadau wataohudhuria katika kongamano hili ni pamoja na watoa huduma za mikopo midogo midogo, benki za wananchi, benki za biashara, benki za ushirika, vyama vya wakulima, wakulima, mawakala wa kilimo, wasomi, serikali za mitaa, watunga sera na wasimamizi wa vyombo vya fedha.


Inategemewa kuwa katika kongamano hili masuala muhimu ya uboreshaji na upatikanaji wa huduma za kifedha vijijini nchini Tanzania yatajadiliwa kwa kina.
Wadau wote wa Huduma za Kifedha vijijini mnakaribishwa kushiriki kongamano hili. Kwa usajili na maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, tafadhali wasiliana kupitia namba na barua pepe zifuatazo :
(1) Simu ya mkononi: +255 764 668 331– Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.
(2) Barua pepe: conference@tamfi.com
Ada ya ushiriki ni Shillingi 100,000 kwa mshiriki ambayo itagharamia huduma zitakazotolewa kwenye kongamano lote.
Malipo yanaweza kufanyika kwa pesa taslimu/hundi kupitia:
TANZANIA ASSOCIATION OF MICROFINANCE INSTITUTIONS
DCB COMMERCIAL BANK
ACCOUNT NO. 0110005000056
WAFADHILI/SPONSORS KWA AJILI YA KONGAMANO HILI
WANAKARIBISHWA. KWA MAELEZO ZAIDI, TAFADHALI WASILIANA NASI KWA NAMBA ZILIZOTAJWA HAPO JUU.
Tanzania Association of Microfinance Institutions
Mtaa wa Uporoto, Barabara ya Bagamoyo,
S.L.P 950,
Dar es Salaam, Tanzania.
Office email address: info@tamfi.com

Pakua

TAMFI ADVERT swahili

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.