TANGAZO MUHIMU KWA WANACHAMA WA TAMFI

CHAGUA WAJASIRIAMALI WANAOKOPA KWENYE TAASISI YAKO KWA AJILI YA SHINDANO LA WAJASIRIAMALI BORA LA CITI 2017

!!!!!!!TUZO KUBWA KUSHINDANIWA!!!!!!!!

 

Mtandao wa Asasi zinazotoa mikopo kwa wajisiriamali wenye biashara ndogo ndogo  (TAMFI) ikishirikiana na  Citi Foundation itatoa zawadi kwa wajisiriamali katika mpango unaojulikana kama  “Citi Micro entrepreneurship Awards  (CMA).” Mpango huo utatoa fursa kwa asasi ambazo ni wanachama wa TAMFI kuchagua wanachama /wakopaji kutoka kwenye taasisi zao ambao watashindanishwa na hatimaye kupata washindi 16.  Zaidi ya Millioni 70 za Kitanzania zitashindaniwa.  Mshindi atapatikana kupitia mchuano mkali. (1) Mshindi wa kwanza atajipatia usd 7500, (2) Mshindi wa pili (usd 6000), (3) Mshindi wa tatu (usd 4000), (4)  Mshindi Mwanamke (2000), (5) Mshindi Kijana (2000), (6) Mshindi Mlemavu (2000), (7) MFI yenye ubunifu ( 1,500), (8) Washindi wengine kumi ambao watapata usd 1000 kila mmoja, na (9) Afisa Mkopo wa Mshindi wa Kwanza ( 1,500).

 

Nani anaweza kushinda tuzo?

Mjasiriamali yeyote anayekopa kutoka kwenye taasisi ya mikopo iwe ni MFI, Benki ya Biashara, Benki ya Jamii, Benki ya Microfinance, SACCO au VICOBA anaweza kushindania tuzo. Taasisi husika itamtambua mjasiriamali bora ambaye anaweza kushindanishwa kwenye huu mchakato wa zaidi ya TZS 70,000,000. Wanawake, Vijana & watu wenye ulemavu watapewa kipau mbele.

 

Nini masharti ya tuzo?

Ni lazima mjasiriamali anayeshindanishwa awe na vigezo mbalimbali kwenye biashara yake, kwenye jamii inayomzunguka, na kwenye familia yake. Vigezo vitakavyozingatiwa  ili mjasiriamali aweze kuingia kwenye shindano hili ni kama inavyoainishwa hapo chini. Mifano halisi itolewe kwenye kila kipengele.

  • BIASHARA INAKUA? Historia ya biashara , ilianza lini, mtaji wa kiasi gani, biashara imeongezeka na kukua kwa kiasi gani, matawi ya biashara yamefunguliwa, faida imeongezeka, masoko yamepanuka n.k
  • KUNA UBUNIFU? Jambo ambalo linafanywa tofauti na biashara zingine. Biashara inatumia teknologia ya habari, mawasiliano na matumizi bora ya nishati.
  • BIASHARA INATOA FURSA ZA AJIRA NA KUKUZA AJIRA? Biashara  imeajiri watu wangapi na imeongeza wafanyakazi wangapi tangu biashara ilipoanza. Na pia kama biashara inazingatia jinsia
  • NINI MCHANGO KWENYE FAMILIA, na JAMII KWA UJUMLA? Mafanikio ya biashara yameleta maendeleo kwenye familia kwa mfano : nyumba, afya, elimu, mazingira n,k
  • MATUMIZI NA NIDHAMU KATIKA MASUALA YA KIFEDHA YAKOJE? Masuala ya kujiwekea akiba na kulipa mkopo, pamoja na nidhamu katika matumizi ya kifedha
  • BIASHARA INA MAENDELEO ENDELEVU? Biashara inaweza kulipa gharama za uendeshaji na kupata faida ya kuendela. Biashara inaweza kuendelea hata kama mwanzilishi hayupo.

 

Maombi yatawakilishwa vipi?

Baada ya Taasisi kutambua wajasiriamali wawili walio bora, itajaza fomu iliyoambatanishwa na kuituma TAMFI kabla/siku ya 31st October, 2017.

TAFADHALI BONYEZA HAPA KUPATA FOMU:Citi Awards application forms

Tafadhali sana tuma pamoja na picha za mjasiriamali anayeshindanishwa hasa ambazo yuko kwenye biashara yake.

KUMBUKA KWAMBA MJASIRIAMALI UTAKAYEMSHINDANISHA KWENYE TUZO HII ANASHINDANA NA WAJASIRIAMALI BORA KUTOKA TAASISI ZINGINE. HIYO NI MUHIMU UKAJAZA FOMU KWA UMAKINI NA KWA KUVUTIA.

 

Tutajuaje kwamba Taasisi yetu imeshinda?  

Baada ya kupitia maombi yote yatakayowakilishwa, kutakuwepo na mchujo wa kwanza. Wajasiriamali hawa watachukuliwa video na picha ambazo zitapitiwa na jopo la majaji na kukubaliana washindi. Washindi watatangawa kwenye sherehe maalum itakayoandaliwa na TAMFI wakishirikiana na CITI BANK Tanzania, mwezi Novemba 2017.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

 

Executive Secretary,

TANZANIA ASSOCIATION OF MICROFINANCE INSTITUTIONS (TAMFI)

54A UPOROTO STREET, OFF BAGAMOYO ROAD,

P.O.BOX 950,

DAR ES SALAAM

Mobile: +255 764 668 331 and +255 752 251 188

Email: info@tamfi.com

Similar Articles

FINANCE AND PLANNING MINI... With the theme of Rural Finance and Agricultural Transformation in Tanzania, the conference kicked off yesterday 13th July 2017 at Julius Nyerere International Convention Center, Dar es
IMPORTANT NOTICE TO TAMFI... NOMINATE CLIENTS FOR THE BEST CITI MICRO ENTREPRENEUR OF THE YEAR AWARDS AMAZING PRIZES TO BE WON Tanzania Association of Microfinance Institutions in collaboration with Citi Bank
Agricultural value chain ... The training was conducted for two and a half days at Kingway Hotel located alongside Dar es Salaam – Mbeya Highway within Morogoro Municipality. The training was
Citi Bank Tanzania CEO sp... CITI MICROENTREPRENEURSHIP AWARDS – CMA 2015 for Tanzania Award Ceremony at the Hyatt Regency, Dar es Salaam September  27, 2016 Speech by  Mr Joseph Carasso – CEO Citibank Tanzania Citibank
31 shortlisted for Citi ... Early this year, Citi Bank launched Citi Micro-Entrepreneurship Awards Program in Tanzania. The awards program is designed in raising awareness about microfinance among micro entrepreneurs who benefit
Members of Tanzania Insti... Addressing TAMFI members in Dar es Salaam, Ms Audrey Linthorst, Lead Africa Analyst of Microfinance Information Exchange (MIX) based in Washington DC said sharing information with peers,
Call to Register for the ... Do you want to participate in  “Rural Finance and Agricultural Transformation in Tanzania” Join us at The 3rd Rural and Microfinance Forum 2017 Date:   13th –
TAMFI: Address Microfinan... *Customer centricity, innovation way forward Failure in financial inclusion in Tanzania can partly be attributed to internal weaknesses of providers of financial services ranging from products costs, packaging,
Notice for TAMFI Annual G... TANZANIA ASSOCIATION OF MICROFINANCE INSTITUTIONS (TAMFI) P. O. BOX 950 DAR ES SALAAM www.tamfi.com NOTICE IS HEREBY GIVEN THAT the 2nd Annual General Meeting of the Members
NATIONAL MICROFINANCE POL... NATIONAL MICROFINANCE POLICY 2017 OCTOBER, 2017 Policy – Fedha English 3

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *